3 Smoothie za kukusaidia tatizo la kuvimbiwa/kuvimba kwa Tumbo.
Smoothie hizi zinasaidia watu wote wenye tatizo la kuvimba kwa tumbo na viungo hivi vya smoothies vina vitamini na madini kama vile vitamin A,B6 na C pia madini ya kalcium na chuma ambayo yanayosaidia mmeng’enyo wa chakula ,kupunguza gesi na kukupa afya ya utumbo.
1. Cucumber – Mints Smoothie

Viungo
- 1 Tango
- Tangawizi vipande vidogo
- Majani ya mchicha robo kichanga
- Majani ya mints kiasi
- 1 Kijiko cha unga wa chia seeds
- ½ Kikombe cha maji ya limau
- 1 Kikombe cha maji ya nazi/dafu
- 1 Kikombe cha maji ya baridi.
2. Papaya – Orange Smoothies

Viungo
- ½ Papai
- Majani ya mchicha kiasi
- Majani ya Coriander kiasi.
- Mbegu za chia seeds
- Tangawizi vipande vidogo
- ½ Kikombe cha maji ya limau
- ½ Kikombe cha maji ya machungwa au Machungwa mawili.
- 1 Kikombe kikubwa cha maji ya baridi.
3. Turmeric – Ginger Smoothies

Viungo
- 1 Tangawizi kubwa
- 1 Manjano kubwa
- ½ Tango
- 2 Kiwi
- Majani ya Cilantro kiasi
- ½ Kikombe cha maji ya limau
- 1 Kikombe cha maji ya baridi
Kumbuka; Jinsi ya Kutengeneza Smoothies hizi
Changanya viungo vyote katika blender yako na sanga mchanganyiko huo hadi uwe laini.Mimina kwenye glass na kunywa.
Hitimisho
Pamoja na kunywa smoothies njia nyingine za kukusadia kukabili tatizo la kuvimba kwa tumbo ni kunywa maji mengi,kufanya mazoezi ,epuka kula vyakula vyenye gesi kama vile maharage, kabichi na viazi, kula mko kamili na pia epuka kula milo mikubwa.
Ni muhimu kushauriana na daktari ikiwa kuvimba kwa tumbo linaendelea au linasababisha maumivu makali.Daktari ataweza kufanya uchunguzi na kupendekeza matibabu sahihi kulingana na sababu ya kuvimba.