Utangulizi
Kwanza kabisa ni muhimu kuelewa kwamba ngozi ni kiungo kikubwa cha mwili ambacho kina jukumu muhimu katika kulinda mwili dhidi ya vijidudu na athari za mazingira. Utunzaji sahihi wa ngozi unaweza kusaidia kudumisha kinga ya mwili na kupunguza hatari ya maambukizi ya ngozi. Aidha, utunzaji wa ngozi unaweza kusaidia katika kudumisha unyevu wa ngozi na kuzuia matatizo kama vile ukavu na kuchubuka.
Kuwa na ngozi yenye afya, yenye kung’aa na yenye uzuri wa asili ni lengo la wengi na linapokuja suala la kutunza ngozi kuna mambo mengi ya kuzingatia,kama mazoea ya kusafisha na kutunza ngozi (skin care routine),mlo na mtindo wa maisha. Hapa nitazungumzia baadhi ya vidokezo muhimu vya kutunza ngozi ili kupata ngozi yenye kung’aa:
Osha uso mara mbili kwa siku.
Kwanza kabisa, ni muhimu sana kudumisha usafi wa ngozi. Ni vyema kuosha uso mara mbili kwa siku kwa kutumia kutumia sabuni laini au gel ya uso ili kuondoa uchafu, mafuta na uchafu mwingine ambao unaweza kusababisha ngozi kuchafuka. Muda mzuri wa kuosha uso ni asubuhi na usiku kabla ya kwenda kulala.
baada ya kunawa tumia rose water au toner ili kusawazisha pH ya ngozi na kuandaa ngozi kwa hatua inayofuata.
Moisturizing
Unyevu wa ngozi ni muhimu pia. Tumia mafuta yanayofaa kwa aina yako ya ngozi ili kudumisha usawa wa unyevu wa asili wa ngozi yako, kuzuia ukavu wa ngozi na kudumisha ngozi yenye afya na yenye kung’aa.
Tumia mafuta yanayo kulinda na jua.
Tumia mara kwa mara mafuta yanayo kukinga na jua yenye wigo mpana na SPF 30 au zaidi ili kulinda ngozi yako kutokana na mionzi hatari ya jua ambayo inaweza kusababisha madhara kama vile kupigwa na jua na hata kansa ya ngozi. Pia, kuvaa kofia na mavazi yenye kujilinda dhidi ya jua inaweza kusaidia kulinda ngozi yako wakati unapokuwa nje.Mafuta haya yanafahamika kama sunscreen au sunlotion.
Exfoliating
Kwa kawaida ngozi kujisafisha yenyewe,kuondoa seli za ngozi zilizokufa kila baada ya week saba hadi kumi.Hii inategemea na afya ya ngozi yako au afya ya mwili wako kwa ujumla.Hivyo ni vizuri kuisadia ngozi kutimiza zoezi hili kwa kufanya exfoliate.
Exfoliating ili ni zoezi la kutumia bidhaa za kuondoa seli za ngozi zilizokufa mara 2-3 kwa wiki, husaidia kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kufanya ngozi iwe nyororo na yenye kung’aa.
Pia kutumia bidhaa za face mask za asili kama liwa,manjano na udongo (clay mask)bidhaa hizi hupenya ndani ya ngozi na husaidia kusafisha ndani na nje ya ngozi.
Kula mlo kamili na wenye afya
Jumuisha matunda mengi, mboga, protini zenye afya, na mafuta yenye afya katika mlo wako. Vyakula vyenye vyenye virutubisho kama vile vitamin C,vitamin E ,beta-carotene na vyakula vyenye antioksidanti (antioxidant)kama vile matunda ya beri,machungwa, majani ya kijani, na karanga vinaweza kusaidia kulinda ngozi yako kutokana na uharibifu unaosababishwa na radicals huru na vinaweza kusaidia katika kudumisha afya ya ngozi na kupunguza hatari ya kuzeeka mapema.
Pia uepuka mazoea ya kunywa pombe kupita kiasi na uvutaji sigara, kwani mazoea haya yanaweza kuharibu afya ya ngozi.
Kunywa maji ya kutosha
Kunywa maji ya kutosha ni muhimu kwa afya ya ngozi yako.Kunywa maji ya kutosha kila siku husaidia katika kudumisha unyevu wa ngozi na kusaidia katika kuondoa sumu mwilini na husaidia katika kuifanya ngozi iweze kung’aa, hivyo hakikisha unakunywa maji mengi kila siku.
Kupata usingizi wa kutosha
kulala kwa wakati ni jambo zuri,Lengo ni kupata masaa 7-9 ya usingizi wa ubora kila usiku ili kuruhusu mwili wako kufanya ukarabati na kurejesha ngozi yako.
Mazoezi ya kupunguza mawazo na mafadhaiko
Kufanya mazoezi ya kupunguza mawazo na mdhaiko ni mazuri sana kwa ngozi, kama vile yoga, mazoezi ya kupumua au mazoezi ya kutuliza akili yanaweza kusaidia kupunguza mafadhaiko na kuimarisha afya ya ngozi yako.
Hitimisho
Kwa kufuata vidokezo hivi na kujumlisha utunzaji wa ngozi katika maisha yako ya kila siku, unaweza kuwa na ngozi yenye afya, yenye kung’aa na yenye uzuri wa asili. Kumbuka kila mtu ana aina tofauti ya ngozi, hivyo ni muhimu kuchagua bidhaa na mazoea ambayo yanafaa kwa aina yako ya ngozi ,pia chagua bidhaa zenye viungo vya asili na zisizo na kemikali kali kwa afya ya ngozi yako.