Utangulizi
Wakati watu wengine wanafanya jitihada za kupunguza uzito, kuna wengine wanajitahidi kuongeza uzito unaofaa, kuongeza uzito inaweza kua ni changamoto sana husasani kwa watoto wadogo. Moja wapo ya njia ya kuongeza uzito ni kula vyakula vyenye wanga , mafuta (fats) na kalorii , Pia kunywa smoothie yenye mchanganyiko wa matunda na viungo vyenye lishe hizo.
Ifuatayo ni moja ya recipe ya smoothie kwa ajili ya kuongeza uzito salama.
Viungo
- 1 Ndizi kubwa
- 1 Parachichi lililokatwa na kutolewa mbegu
- 1/2 Kikombe cha tui la nazi
- 2 Vijiko vya karanga iliyosangwa ( peanut butter)
- 1 Kikombe cha maziwa ya mtindi au maziwa ya kawaida
- 1 Kijiko cha asali
- 1/2 Kikombe cha maji baridi.
Jinsi ya kutengeneza
- Kata ndizi na parachichi, na kuweka katika blender
- Ongeza karanga (peanut butter)
- Ongeza maziwa na tui la Nazi kwenye blender yako
- Ongeza asali na maji katika mchanganyiko wako
- Kisha funga blender yako na saga mchanganyiko huo hadi uwe laini
- Onja Kama umeupenda mchanganyiko wako na Kama una hitajika ongeza viungo zaidi kulingana na ladha yako
- Kama umeipenda mimina smoothie yako kwenye glass na kunywa .
Hitimisho
Kunywa smoothie hii mara moja au mara mbili kwa siku na utafanikiwa kuongeza uzito kwa haraka , Pia usisite kubadilisha matunda na viungo vingine ili upate ladha tofauti tofauti ya smoothie ili mradi tu uzingatie aina ya matunda na viungo vyenye lishe ya wanga ,mafuta (fats) na na kalorii kwa wingi. .