Njia 9 za kukusaidia kusafiri kwa bajeti ya chini.

Kusafiri kunaweza kuwa ghali. Wakati mwingine hakuna chaguo lingine ila kusafiri na hivyo inaweza isiwe kitu ambacho unataka kutumia pesa nyingi juu yake. Kuna baadhi ya njia unaweza kutumia ili kuokoa pesa unaposafiri na bado ukafurahia safari yako.

  1. Andaa bajeti 

Jambo la kwanza kufanya ni kuandaa bajeti yako,bajeti hii ujumuishe gharama zote kama gharama za usafiri,malazi(hoteli),chakula,gharama za kulipia maeneo ya utalii utayakotembelea n.k.Jumlisha gharama hizo kulingana na siku utakazo kaa katika mji unaotembelea bajeti hiyo itakusaidia kujua ni sehemu gani unaweza kubana matumizi,au ni siku ngapi unaweza kuafford kukaa katika mji huo.

  1. Zingatia muda wa kusafiri.

Epuka kusafiri kipindi ambacho watu wengi wapo kwenye likizo au mapumziko, kwani kipindi hicho ndio bei zinakua juu kwa sababu watu wengi wanatembelea maeneo ya vivutio.

  1. Kulinganisha ndege

Moja ya gharama kubwa za awali wakati wa kusafiri ni tiketi ya ndege,Kwa hivyo,ili kusafiri kwa bei nafuu tumia tovuti kulinganisha bei za ndege kama vile kiwi,au nunua moja kwa moja kupitia kampuni ya ndege .Pia epuka kununua tiketi nyakati za mwisho au siku chache kabla haujasafiri kwani bei inakua kubwa zaidi.

  1. Tumia usafiri wa umma

Unapokuwa ndani ya mji au sehemu unayotembelea badala ya kutumia teski au usafiri wenye gharama tumia public transport kama vile mabasi,treni au tumia bajaji(tuk-tuk),bodaboda,baiskeli kutoka sehemu moja kuenda sehemu nyingine, Unapoamua kuchukua usafiri huu utaokoa pesa hiyo,lakini pia utapata fursa ya kuona miji mingine unapokuwa njiani na kuona vivutio vingine vya utalii wa ndani na utaweza kutengeneza urafiki na wenyeji.

  1. Kula Kama Wenyeji

Epuka kula kwenye migahawa ya watalii na kula katika migahawa ya wenyeji kwa chakula cha bei nafuu na cha utamaduni, na kama unaishi kwenye hostel au Airbnb mara nyingi wanaruhusu kutumia jiko hivyo pika chakula chako mwenyewe.

  1. Tafuta Malazi ya Bei Nafuu

Angalia hosteli,nyumba za wageni au Airbnb kwa malazi ya bei nafuu badala ya hotel za kifahari.Pia unaweza kuomba kuishi nyumbani kwa ndugu au rafiki anaeishi mji huo,hii haitakusaidia kusave pesa tu bali itakuasadia kujua maeneo mazuri zaidi ya kutalii.

  1.  Fanya Utalii wa Bure

Tembelea vivutio vya bure kama mbuga za umma,masoko ya mitaani na matukio ya bure.Pia fanya utafiti na zidhatia siku ambazo ni bure kutembelea hifadhi za taifa, kwa mfano kila mwaka hifadhi ya taifa ya Marekani inatoa siku kadhaa za kuingia bure siku ya Martin Luther King Jr. mwezi wa kwanzai na siku ya wananchi wa taifa mwezi wa nne.

  1. Pack Vyakula na Nguo za Kutosha

Kumbuka kupaki nguo na vyakula vya kutosha hususani kama unasafiri na familia na unafikia kwenye nyumba ya Airbnb ambayo wanaruhusu kutumia jiko,pia kumbuka kupack nguo kulingana na hali ya hewa ya mji huo hii itakupusha na gharama za kununua nguo mpya.

  1. Chagua Nchi Zenye Gharama Nafuu

Chagua nchi zenye gharama nafuu za malazi na makazi kama Vietnam, Thailand,Morocco n.k nchi hizi zina vivutio vizuri na hazina gharama kubwa.

Hitimisho

Kusafiri kwa bajeti ndogo ni jambo linalowezekana na linaloweza kuleta furaha, mradi mipango ya makini na maamuzi ya busara yanachukuliwa.Pia, kujua vipaumbele vyako na kuwa na uvumilivu kunaweza kusaidia kuepuka gharama zisizo za lazima. Hatimaye, kusafiri kwa bajeti ndogo si tu kuhusu kuokoa pesa, bali pia ni kuhusu kuthamini zaidi safari na uzoefu unaopatikana njiani.

About Author
Maua Salim
View All Articles
Check latest article from this author !
DEBLOATING SMOOTHIES RECIPES
CLEANSING PRODUCTS FOR DIFFERENT TYPES OF SKINS
SMOOTHIES FOR PREGNANT WOMEN